Thursday 14 March 2013

Joho atangazwa mshindi - Governor Mombasa

Aliyekuwa mbunge wa Kisauni na Waziri msaidizi wa uchukuzi Mhe. Hassan Joho ndio Gavana mteule wa Jimbo la Mombasa. 












Joho mwenye alimshinda mpinzani wake wa karibu Suleiman Shahbal wa Wiper ame toa wito kwa aliyo wa shinda kushirikiyana naye kuendeleza mji wa Mombasa kwasababu anadai Mombasa ni Kubwa mnoo na hataweza hiyo kazi mwenyewe.

Hata kabla Joho kuvuta pumvi, mpinzani wake ambaye wako kwenye mrengo moja wa CORD ame pinga vikali ushindi wa Joho na ame enda Kortini kupinga ku apishwa kama Gavana wa Jimbo La Mombasa.

Shahbal anadai kwamba uchaguzi wa Mombasa ulikuwa na tashwishi nyingi na ana omba mahakama iamrishe kura ya Mombasa iregelewe.

Raila na CORD kuenda cortini kupinga maamuzi ya wa Kenya


MGOMBEA urais wa muungano wa CORD Raila Odinga amesema atapinga ushindi wa Uhuru Kenyatta wa Jubilee kortini. Amesema kuna makosa mengi katika ujumlishaji wa kura na kutoa wito kwa wafuasi wake wawe watulivu na kudumisha amani anapotafuta usaidizi Mahakama ya Juu.









MGOMBEA urais wa muungano wa CORD Raila Odinga amesema atapinga ushindi wa Uhuru Kenyatta wa Jubilee kortini. Amesema kuna makosa mengi katika ujumlishaji wa kura na kutoa wito kwa wafuasi wake wawe watulivu na kudumisha amani anapotafuta usaidizi Mahakama ya Juu.


Bw Kenyatta alipata kura 6,173,433 kati ya jumla ya kura 12,338,667 zilizopigwa katika uchaguzi huo wa Jumatatu ambazo ni asilimia 50.03 ya kura.
Bw Odinga aliibuka wa pili na kura 5,340,546 ambazo ni asilimia 43.28  ya kura zilizopigwa.

Alhamisi, muungano wa Coalition for Reforms and Democracy (Cord) ulikuwa umeitisha kusimamishwa kwa uhesabu wa kura ukisema shughuli hiyo ilikuwa ya kutiliwa shaka.
Kalonzo Musyoka, aliyekuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga, alisema Tume Huru ya Muda ya Uchaguzi (IEBC) inafaa kulaumiwa.

Uhuru ndio Chaguo la Wakenya

Terehe 4 Marchi 2013 Wakenya walienda debeni ku amua uongoze wake mpya. 

Upinzani wakaribu kabisa ulikua baina wa Uhuru Muigai Kenyatta wa mrengo wa Jubilee na Waziri mkuu Raila Amolo Odinga wa mrengo wa CORD.

JUMLA ya matokeo kutoka maeneo bunge yote (291/291): Uhuru 6,173,433 (50.07%); Raila 5,340,546 (43.28%). Jumla za kura zilizopigwa 12,338,667.

Kutoka kwetu tunamtakia Rais Uhuru Kenyatta na mrengo wake wa Jubilee mema kuendeleza nchi yetu mbele.

Friday 23 November 2012

Demokrasia ya CCM TANZANIA imepita viwango vya kimataifa


TUMESHUHUDIA Mkutano Mkuu wa nane wa CCM ukimalizika kwa kuwapata viongozi wa juu wa chama hicho na kuhitimisha chaguzi zake za ndani zilizoanzia kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.

Baada ya mkutano huo, chama hicho kupitia Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimeunda Sekretarieti mpya iliyosheheni vigogo wanaotarajiwa kukivusha kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Pia mkutano huo umewachagua viongozi wa juu, akiwamo Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete akisaidiwa na wenyeviti wawili, Philip Mangula wa Bara na Rais Ali Mohamed Shein wa Zanzibar.
Nafasi ya Katibu Mkuu amepewa Abdulrahman Kinana akisaidiwa na Mwigulu Nchemba (Bara) na Vuai Ali Vuai (Zanzibar).
Wajimbe wengine wa Sekretarieti ni Dk Asha Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa), Zakhia Meghji (Uchumi na Fedha), Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni) na Nape Nnauye anayeendelea na nafasi yake ya Itikadi na Uenezi.
Mengi yamesemwa kuhusu safu hiyo. Mimi kwa upande wangu najikita zaidi kwenye njia iliyotumika kuwapata viongozi hao na jinsi mfumo wa demokrasia unavyofinywangwa na chama ili kupata viongozi wake.
Kwanza nianze na jinsi nafasi ya mwenyekiti iliyogombea na Rais Jakaya Kikwete peke yake na tunaambiwa kuwa ameshinda kwa asilimia 99.92.
Kabla hata mkutano huo haujaanza, kulionekana vipeperushi vikimtaka Rais Kikwete asigombee nafasi hiyo kwa maelezo kuwa ingekuwa vyema apunguziwe majukumu kwa kutomhusisha na uongozi wa chama na Serikali kwa wakati mmoja.
Hata hivyo, kwa kuliona hilo, mikakati iliwekwa ili kundi linaloonekana kumpinga mwenyekiti lidhibitiwe.
Hata ilipofika siku ya uchaguzi, ilibidi Katibu Mkuu wa zamani, Yusuf  Makamba aalikwe jukwaani kueleza umuhimu wa kuendelea na uenyekiti wa Rais Kikwete.
Makamba kama kawaida yake akitumia Biblia na Qur’an alimnadi vyema Rais Kikwete huku akivuna sifa nyingi kutoka kwa makada wa chama hicho na kutumia nafasi hiyo kulaani walioandaa mpango huo ulioitwa ‘kura za maruhani’.
Wakati wa uchaguzi, utaratibu mpya uliwekwa ambapo wajumbe sasa walitakiwa kupiga kura kwa mikoa yao. Ili ikitokea mkoa fulani umempinga Rais Kikwete basi wajue namna ya kuufinya huko baadaye.
Njia zote hizo ziliwafanya watu wenye mawazo mbadala, kunywea na kulazimika kupiga kura zote kwa Rais Kikwete.
Haikuwa rahisi kupata asilimia 99.92, ilibidi mikakati ifanyike kama hivyo. Hivyo hivyo kwa makamu wenyeviti yaani Philip Mangula na Dk Ali Mohamed Shein waliopata asilimia 100. Unaambiwa hakuna hata kura moja iliyoharibika.
Kwa kweli hii ‘ni demokrasia iliyovuka mipaka ya kimataifa’. Yaani ndiyo kusema kuwa ndani ya CCM hakuna mawazo mbadala? Au hakuna watu wanaotaka fulani awe mwenyekiti badala ya Rais Kikwete au makamu wake Dk Shein, au Mangula?
Mimi siamini, maana yake ni kama vile kura zilipigwa na ‘robot’. Siamini kwa sababu kwanza tangu awali kulikuwa na vipeperushi vikiwashawishi wajumbe kutomchagua Rais Kikwete bali mtu mwingine, japo hatajwi.
Vilevile kutokana na mikakati iliyowekwa katika uchaguzi huo nayo inaleta mashaka.
Ndiyo kusema safu hiyo iliyowekwa CCM ilikuwa ya kimkakati na ilihitaji tu baraka za wanachama.
Utaratibu huu wa kusimamisha mtu mmoja kugombea bila kuwepo mtu wa pili wa kumshindanisha naye ndiyo ule uliokuwa ukitumiwa na Mwalimu Nyerere baada ya kuvunja vyama vya upinzani mwaka 1965.
Pamoja na mema mengi aliyofanya Mwalimu Nyerere, ukweli ni kwamba hakupenda upinzani wala mawazo mbadala. Ndiyo maana katika chaguzi zote ziwe ndani ya chama au uchaguzi mkuu aligombea yeye peke yake na kivuli hadi alipong’atuka mwaka 1985.
Kwake ilikuwa ni ‘zidumu fikra za mwenyekiti wa chama’.  Huo ndiyo utamaduni unaoendelea ndani ya CCM, hata kama wanachama hawamtaki mwenyekiti basi demokrasia inafinyangwafinyangwa huku ikitiliwa maneno matamu ya kina Makamba, ndipo mwenyekiti anapatikana.
Hakuna ushindani wa kweli, hakuna uwazi, hakuna usawa.
Hili haliko CCM tu, hata baadhi ya vyama vya upianzani mambo ni hayo hayo, viongozi wameshawekwa, halafu usanii tu unafanywa ili kuwapitisha.
Kuna baadhi ya vyama vya siasa, tangu vilipoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1990, viongozi ni wale wale miaka nenda rudi.
Lakini kwa kuwa CCM ni chama kikongwe, basi kingepaswa kutoa somo le demokrasia kwa vyama vingine.
Vyama vya siasa vinapaswa kuonyesha demokrasia ya kweli ndani yao kabla ya kwenda kushindana na vyama vingine. Kama viongozi wa vyama watavumilia kushindwa ndani ya vyama hivyo basi watajenga utamaduni wa kuvumilia hata matokeo ya uchaguzi mkuu. Ila kama hayo yanashindikana ndani ya vyama, pia ni ndoto kuwa na demokrasia ya kweli nchini.
Elias Msuya ni mwandishi wa makala wa gazeti la Mwananchi; 0754 897 287

Umaarufu wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete waporomoka


KUONGEZEKA kwa matukio ya rushwa nchini kumesababisha umaarufu wa Rais Jakaya Kikwete kushuka kwa asilimia 20 katika miaka minne iliyopita, utafiti mpya unaonyesha.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini (REPOA) kati ya Mei na Juni 2012 unaonyesha kwamba kiwango cha Rais Kikwete kukubalika kimeshuka kutoka asilimia 90 mwaka 2008 hadi asilimia 71 mwaka huu.

Pia, mwaka huu watu saba kati ya kumi walioshiriki katika utafiti huo waliihusisha ofisi ya Rais kwa rushwa na kwamba hali hiyo ni tofauti na mwaka  2008 ambapo walikuwa  watu watano kati ya 10, utafiti huo ulieleza.

Rais Kikwete ambaye hivi karibuni alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa CCM, wakati akizungumza na mamia ya makada wa chama hicho Dar es Salaam alikiri kwamba watu wengi wamepoteza imani na  chama hicho kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa na ufisadi.

Katika maelezo yake, Kikwete alisema kuwa ni lazima kurejesha imani ya wananchi kwa chama hicho na kufanya uchunguzi ili kujua wapi kilipokosea.

Utafiti huo ujulikanao kama Afrobarometer Tanzania, uliotolewa jana Dar es Salaam pia umeonyesha kuwa asilimia 90 ya watu waliohojiwa hawakuridhika na utendaji kazi wa Rais kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Utafiti huo ni mfululizo wa tafiti linganishi zinazohusisha tabia ya jamii unaofanywa katika nchi 35 barani Afrika kati ya mwaka 2011 hadi 2013.

Afrobarometer  ni utafiti unaoonyesha  mitazamo ya umma juu ya demokrasia na mbadala wake, tathmini ya ubora wa utawala na utendaji wa kiuchumi.

Akiwasilisha ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Huduma ya Utafiti wa Repoa, Jamal Msami  alisema kwa wastani mwaka 2012 watu wengi zaidi waliishutumu Serikali kushindwa kuimarisha uchumi wa nchi kuliko ilivyokuwa mwaka 2008.

Alisema kuwa katika utafiti huo watu wengi walizungumzia kuporomoka kwa uchumi wa nchi na uhaba wa vyakula vya aina mbalimbali pamoja na kuwapo kiwango cha utoaji wa huduma kwa jamii kutoridhisha.

"Kwa ujumla, tafiti inatoa taswira hasi kwa utendaji wa Serikali katika nyanja zote kwa kipindi hicho cha miaka minne," alisema.

Licha ya tathmini ya utendaji mbaya wa Serikali, Watanzania bado wana matumaini ya kuwa Serikali itaweza kutatua mambo muhimu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema kuwa Watanzania walipoulizwa juu ya uwezekano wa Serikali kutatua matatizo muhimu zaidi, asilimia 66 ya waliohojiwa walionyesha kuwa na imani kwamba inaweza, kiwango ambacho ni tofauti na cha 2008 ambapo mtu mmoja kati ya kumi ndio alionyesha kutokuwa na imani na jambo hilo.

Katika ngazi ya kitaifa, asilimia 8 ya watu wazima walisema kuwa watoto wao walipewa chakula wakiwa shuleni, katika mpango unaoendelea nchini wa chakula bure shuleni.

Alisema  katika utafiti huo asilimia 66 ya watu wazima waliulalamikia ubora wa ufundishaji wa wanafunzi katika shule za msingi, kwamba utafiti wa mwaka huu unatoa misingi muhimu na ya kutosha kwa ajili kufikiri upya mikakati ya utendaji katika kukuza ubora wa ufundishaji.

Alisema kuwa tafiti za mwaka 2008 na mwaka huu zinaonyesha hali halisi ya maisha waliyonayo Watanzania.

"Si jambo la kushangaza kama karibu theluthi mbili (asilimia 64) ya Watanzania watu wazima hawakuwa na kazi ya kuwawezesha  kulipwa mshahara yao, ikilinganishwa na asilimia 56 mwaka ya  2008," aliongeza.

Alisema asilimia 53 na 54 ya watu waliohojiwa katika kipindi cha utafiti huo walisema kuwa katika kipindi cha miaka minne, tangu 2008 waliwahi kula mlo mmoja tu kwa siku.

Baadaye akizungumza na waandishi wa habari mara baada kutangazwa kwa matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Profesa Samuel Wangwe alisema licha ya utafiti huo kuonyesha kwamba imani ya umma imepungua kwa Rais, lakini baadhi yao wana matumaini kwamba hali itatengemaa siku zijazo.

Profesa Wangwe alisema kupungua kwa imani ya wananchi kumetokana na matatizo ya kiuchumi licha ya taasisi za fedha za kimataifa kusema kwamba Tanzania inafanya vizuri katika eneo hilo.

“Wananchi wanasema bado uchumi wetu ni tatizo kwa sababu wanadai kuwa maisha bado ni magumu na duni na  hakuna kitu kinachobadilika,” alisema Profesa Wangwe.
dhuru na Shukrani kwa: www.mwanainchi.co.tz 

MWANAMUME ASHAMBULIWA NA KUJERUHIWA NA TUMBILI


John Mwangi
John Mwangi akiwa hospitalini Nyeri anakouguza majeraha baada ya kushambuliwa na tumbili kijiji cha Watuka, Kieni Magharibi. Picha/JOSEPH KANYI 
Na ERIC MUTAI
Mwanamume wa umri wa miaka 44 anauguza majeraha katika hospitali ya mkoa ya Nyeri baada ya kushambuliwa na tumbili katika kijiji cha Watuka wilayani Kieni Magharibi.

MWANAMUME wa miaka 44 anauguza majeraha katika hospitali ya mkoa ya Nyeri baada ya kushambuliwa na tumbili katika kijiji cha Watuka wilayani Kieni Magharibi.
John Mwangi alikuwa ameenda shambani mwake kulinda mimea yake dhidi ya kuharibiwa na tumbili kabla ya tukio hilo.
Akiongea na Taifa Leo katika kitanda hospitalini, baba huyo wa watoto wanne alisema kuwa tumbili mmoja mwenye mwili mnene alimshambulia alipojaribu kumfukuza kutoka shambani.
Alieleza kuwa aliwapata tumbili kadhaa wakisherehekea mimea yake ndipo alipoanza kuwapigia kelele na kuwafukuza akiwa ameandamana na mbwa wake.
Tumbili walitoroka kuelekea msitu mdogo ulio karibu na shamba lake lakini mmoja aliyekuwa mnene hakutoroka bali aliendelea kuangalia Bw Mwangi alivyokuwa akifanya bila kutishika.
“Nilimuangalia kwa muda kwani sikujua nia yake ndipo mbwa wangu akaanza kucheza naye. Nilienda kando kidogo kutafuta fimbo nimfukuze nayo ndipo akaruka mbele yangu na kunishika mikono,” alisema Bw Mwangi.
Tumbili huyo alianza kumuuma mikono Bw Mwangi aliyekuwa akipiga mayowe kwa uchungu aliokuwa anasikia.
Alisema aling’ang’ana lakini tumbili akamzidi nguvu na kumuangusha chini na kuanza kumuuma miguuni na kumkwaruza tumbo kwa kucha.
“Nilikuwa napiga kelele kwani nilihisi uchungu mwingi sana. Alipokuwa ananitafuna miguu nilimrushia teke moja lililompata kwa tumbo ndipo aliniwachilia na kukimbia. Sijawahi kuona wala kusikia jambo kama hilo maishani mwangu,” alisema Bw Mwangi.
Wanakijiji waliosikia mayowe walifika mahali pale kumsaidia na wakampata akiwa anatokwa na damu mikononi na miguuni lakini tumbili alikuwa amekwisha ondoka.
Kufanyiwa upasuaji
Walimkimbiza katika hospitali ya mkoa ya Nyeri alikopelekwa katika chumba cha upasuaji na kudungwa shindano ya kuzuia kuambukizwa ugonjwa.
Bw Mwangi alivunjika mkono wa kulia wakati alipokuwa waking’ang’ana na tumbili.
Alielezea kuwa wanaume hushinda kwenye mashamba wakilinda mimea yao isiharibiwe na tumbili ambao ni wengi katika sehemu hiyo.
Wakati mwingine wanakijiji huwaita maafisa wa wanyama pori (KWS) kuwaondoa tumbili na huwa wanawafukuza hadi katika msitu mdogo ulio karibu. Tumbili hurudi tena kushambulia mashamba maafisa hao wakiondoka.
“Tumbili hao huwa hawaogopi wanawake na watoto. Hata mwanamke afanye nini tumbili hawawezi kumuogopa. Ikiwa wanaweza kumshambulia mwanamume mzima kama mimi, tunashangaa wanaweza kuwafanya nini wanawake na watoto,” alisema Bw Mwangi.
Familia yake ilimtembelea hospitalini na kudai fidia kutoka kwa shirika la KWS, ikisema kuwa wanyama walimshambulia akiwa shambani mwake.
Waliomba wanyama hao waondolewe sehemu hiyo kwani wanasababisha hasara kubwa kwa kuharibu mimea yao .
Aidha wanasema wanahofia maisha yao baada ya kisa kilichompata Bw Mwangi.
Credits: Swahili Hub

Shirika la NTA (National TaxPayers Association) inatoa repoti ya CDF

Shirika la NTA (National TaxPayers Association) imetoa ripoti yake hapo jana ikiweka wazi orodha ya ma eneo bunge zilizo tumia na kufuja pesa ya CDF.

Eneo bunge la Mvita na Eldoret North ikiwa mikononi Mheshimiwa Najib Balala na Mheshimiwa William Ruto ziliorodheshwa kati ya maeneo bunge 210 zilizo tumia pesa yake kwa miradi yanao nufaa wanainchi sanaa na hakuna recodi ya pesa ilio fujwa ama kutotumika.

Yalio orodheshwa ya mwisho ni eneo bunge la Nambale na eneo bunge la Changamwe.

Hivo Hivo ndani ya ripoti yao ina onesha wa bunge wamekuwa wa angalifu sana kuliko mwaka iliopita kwa utumiaje ya pesa ya umma.

Ewe Mwanainchi, Hakikisha kiongozi unaem chagua. Ni haki yako kuchukua Kura na kuweza kuwa na nguvu ya kutimuwa wanasiasa wasio jali mwanainchi na wafujaji wa pesa.

MAAFISA WA POLISI WALIOFARIKI SAMBURU WAFIKA 42


MAAFISA wa polisi waliofariki baada ya kushambuliwa na wezi wa mifugo Baragoi, Samburu Jumamosi wamefika 42 huku kukiwa na dalili huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Shirika la habari la Uingereza, BBC, limeripoti kuwa waliofariki wamefika 41, likinukuu duru kutoka idara za serikali Kenya.
Miili ya waliofariki ilisafirishwa kwa ndege hadi Nairobi huku kamati ya Bunge kuhusu usalama ikiitaka Serikali ichukue hatua kukabili wavamizi wanaodaiwa kutoka Turkana.Thelathini kati ya waliofariki wanadaiwa kuwa askari wa akiba. Maafisa sita bado hawajulikani waliko.
Shambulio hilo dhidi ya maafisa wa polisi ndilo mbaya zaidi kushuhudiwa tangu uhuru.
Septemba, maafisa wanane wa polisi waliuawa katika makabiliano kati ya jamii mbili Tana River na kupelekea operesheni kubwa ya kuwapokonya wakazi silaha.

Mkuu wa Mkoa Bonde la Ufa Osman Warfa, aliyeongoza kundi la maafisa wakuu serikalini kuzuru Samburu alikataa kusema lolote kuhusu shambulio hilo.
Alikuwa ameandamana na mkuu wa polisi wa Bonde la Ufa John M’Mbijiwe. Wakuu hao waliandaa mkutano wa faragha Baragoi kabla ya kurejea makao makuu ya mkoa Nakuru.
Kamishna wa Polisi Matthew Iteere pia alizuru eneo hilo. (SWAHILI HUB)
Manusura na familia ya walipoteza watu wao wanalalamika kuto pata usaidizi wowote kutoka kwa serikalli. 
Ma familia hayo pia wametoka habari muhimu kwamba hawo ma afisa wengi wao ni wale walio fuzu Agosti wa mwaka huu kutoka shule ya kujifunza polisi. Umri ya walio uwawa ina aminika kuwa kati ya 20 hadi 26.

Nihali ya ku sikitisha sana kwa inchi yetu kupoteza walinda usalama wengi kati ya hizi siku ya ma juzi, Anasema Camishna wa polisi Mathew Itere