Friday 23 November 2012

MAAFISA WA POLISI WALIOFARIKI SAMBURU WAFIKA 42


MAAFISA wa polisi waliofariki baada ya kushambuliwa na wezi wa mifugo Baragoi, Samburu Jumamosi wamefika 42 huku kukiwa na dalili huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Shirika la habari la Uingereza, BBC, limeripoti kuwa waliofariki wamefika 41, likinukuu duru kutoka idara za serikali Kenya.
Miili ya waliofariki ilisafirishwa kwa ndege hadi Nairobi huku kamati ya Bunge kuhusu usalama ikiitaka Serikali ichukue hatua kukabili wavamizi wanaodaiwa kutoka Turkana.Thelathini kati ya waliofariki wanadaiwa kuwa askari wa akiba. Maafisa sita bado hawajulikani waliko.
Shambulio hilo dhidi ya maafisa wa polisi ndilo mbaya zaidi kushuhudiwa tangu uhuru.
Septemba, maafisa wanane wa polisi waliuawa katika makabiliano kati ya jamii mbili Tana River na kupelekea operesheni kubwa ya kuwapokonya wakazi silaha.

Mkuu wa Mkoa Bonde la Ufa Osman Warfa, aliyeongoza kundi la maafisa wakuu serikalini kuzuru Samburu alikataa kusema lolote kuhusu shambulio hilo.
Alikuwa ameandamana na mkuu wa polisi wa Bonde la Ufa John M’Mbijiwe. Wakuu hao waliandaa mkutano wa faragha Baragoi kabla ya kurejea makao makuu ya mkoa Nakuru.
Kamishna wa Polisi Matthew Iteere pia alizuru eneo hilo. (SWAHILI HUB)
Manusura na familia ya walipoteza watu wao wanalalamika kuto pata usaidizi wowote kutoka kwa serikalli. 
Ma familia hayo pia wametoka habari muhimu kwamba hawo ma afisa wengi wao ni wale walio fuzu Agosti wa mwaka huu kutoka shule ya kujifunza polisi. Umri ya walio uwawa ina aminika kuwa kati ya 20 hadi 26.

Nihali ya ku sikitisha sana kwa inchi yetu kupoteza walinda usalama wengi kati ya hizi siku ya ma juzi, Anasema Camishna wa polisi Mathew Itere

No comments:

Post a Comment

Ji husishe kwa maoni yako ndio ukweli upatikane kwa manufaa wetu