Sunday, 30 September 2012

Uzinduzi wa Chama cha Ukombozi Cha Pwani Republican Congress Party Of Kenya (RC)

Leo hii, Historia imeingia katika kumbukumbu za ki historia kwamba Pwani ume zinduliwa Chama Kipya ambacho ita ongozwa Na aliyekuwa waziri wa Utalii na Mbunge wa Mvita Najib Balala, Na mwandani wake Ibrahim Khamis Babangida ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha Mombasa county Governor. 


Chama hicho kina itwa Republican Congress Party Of Kenya (RC) na alama yake ni Farasi! 
Farasi kama wenyewe wanavo sema ni mnyama ambaye ni wa nguvu na mwenye uzuri. Farasi huyo atatumiwa ku shindana na mikoa mengine katika nchi ya Kenya ku tetea na kulinda haki ya watu walio dhulumiwa na serikali zilizo pita yaani Marginalized communities. Il hali chama hichi ni National party, Mizizi yake yatakuwa maeneo ya Pwani.

Kwa mtazamo wa wanainchi walio hudhurua uzinduzi huo, wame ona mwangaza, wame ona mwaumko mpya, wameona nyota na wako na imani na chama hicho cha RC. 

Uzinduzi huo uli jumisha watu kutoka sehemu mbali mbali, tabaka mbali mbali nawatu wa kabila zote na watu kutoka nchi nzima ya Kenya. Moja wao akiwa kigogo wa zamani Bwa Jahazi, Masumbuko na Simba Wanje (mzee wa Kaya).

Mwenye kiti wa Chama anaitwa Wycliff Anyasi na naibu wake Ms Lai Khamis.

Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Najib Balala alitangaza kuwa atawania kiti cha Mombasa COunty Senator kwa kutumia tikiti cha RC na aliendelea ku sema kwamba chama cha RC haina haraka kuweka mgombeya wa Urais 2012/13. Mpango wao ni kuji tayarisha kwa uchaguzi wa 2022.

Kwa mtazamo wa wengi chama cha RC ni chama cha wanainchi na hususan watu wa pwani! Watu walio hudhuria na kuji sajili ni wanainchi na wana sema wamechochwa na viongozi hapo wa pwani na hawana haja yao katika chama cha RC.


RC Yawezekana ndio msemo ya chama hicho ikifatwa na alafa ya Farasi.


No comments:

Post a Comment

Ji husishe kwa maoni yako ndio ukweli upatikane kwa manufaa wetu