Showing posts with label Shairi. Show all posts
Showing posts with label Shairi. Show all posts

Monday, 9 April 2012

Shairi Ndugu fanya fahamu - Posted by Viewer

"NDUYANGU FANYA FAHAMU,
USIDHANI KITI CHA MAMBASA NKITAMU,
CHATAKA UTU NA UANADAMU, 
NA DEREVA MKARIMU,

KUIENDESHA KAZI NGUMU,
SAA ZOTE UNA HAMU,
KIHUDUMU SIHUDUMU,
KILA MJA TAKULAUMU,

WENDA UKIMHUJUMU, 
WANENA BALALA NI DHALIMU,
USITIE WATU SUMU,
KIFIKIRI WATAKUREHEMU,

KWA MAENDELEO WAKENYA WAMUHESHIMU,
SIO ETI KWA MANENO MATAMU,
NDUYANGU SIWE HASIMU,
WALA JOKA LA MDIMU,

NAMALIZIA YANGU KALAMU,
NASAHA NAKUPA HUMU HUMU,
SUBIRI UWE MAKAMU,
BADO NI YAKE BALALA ZAMU.

NDUYANGU MOMBASA KUIFAHAMU,
SIASA YAKE YATAKA MWALIMU,
HAWAKUIEZA WENYE AKILI TIMAMU,
WATAIEZA WENDWAZIMU?

Shairi Hayani Hayani- Posted by Viewer

"HAYANI HAYANI WAPWANI, 
NAINGIA UWANJANI,
MAHASIDI JIANDAENI,
KICHAPO NIWAPENI,

...NTAKAYOWAPA SI MATANI,
MTAKIMBILIA VICHAKANI,
HUKU HAMUONI,
WALA KULE HAMUONANI,

SIELEWI IKHIWANI,
BALALA MEWAFANYA NINI,
HAMUMTOI MIDOMONI,
HAJAWAKOSEA MASIKINI,

BALALA HANA UCHINI,
HUYASEMA HADHARANI,
MUKITAKA CHUKUWANI,
HAMUTAKI YAACHANI,

MIAKA ZAIDI YA ISHIRINI,
MVITA TAABANI,
UMEKUJA BALALA MTAANI,
METUTOWA TAABUNI,

WALOKAA MAJUMBANI,
LEO WAMO SHULENI,
MVITA, SHEIKH ABDALLA FARSY ALOJENGA NNANI?
MAKANDE NA MAKUPA ZITAANZA KARIBUNI,

TULIFELI SHULENI,
MIAKA YA ZAMANI,
LEO TUNA THAMANI,
TUMEFUZU MITIHANI,

SIJAFIKA KIKOMONI,
NAENDELEA WANDANI,
TUPITE KIVUKONI,
WALL YA PILI TUANZENI,

Shairi kutoka moyoni - Posted By Viewer


NALOANDIKA NI YAKINI,

HAYANITOKI KINYWANI,
BALI KIFUANI,
NDANI MWANGU MOYONI,

......WALLAHI SINASIRI,
BALI NINAJIBU,
NASEMA KWA DHAHIRI,
HUU NI WANGU WAJIBU,

TAIBU LIJARIBU,
KUMPINGA NAJIBU,
KURA TULIPO HISABU,
KANYAMAA KAMA BUBU,

KAKIMBIA KWA AIBU,
MOMBASA KAIGHIBU,
ALISHIKA YAKE ADABU,
KAMWE TENA HATOJARIBU,

SASA NI MWANASHARIFU,
AJIGAMBA KIJISIFU,
MEANZA KWA PUPA ALIFU,
SIASA ZA UVUNDIFU,

BWANA HUYU MEDANGANA,
PESA AZIMIMINA,
HAPA LEO KULE JANA,
ENDA KIWAGHURI VIJANA,

AMEKUJA KWA HASIRA,
AFIKIRI MASIHARA,
HEBU FANYA BUSARA,
SIJE UKENDA HASARA,

MEINGIA KWA KIBURI,
YUWASEMA ANASIRI,
WAMVITA HATUTAKI SIRI,
TWATAKA LILO DHAHIRI,

BALALA KUWA GAVANA,
NI HAKI YAKE BWANA,
AMEFANYA YA MAANA,
DHAHIRI YAONEKANA,

NIKISEMA HOYEE,
SEMENI HOYEE,
BALALA HOYEE,
SOTENI HOYEE."

Shairi La ma Hasidi - Posted By Viewer


BISMILLAHI LEO NAANZILIA,

PILI MTUME NAMSWALIA,
MATO YA HASIDI YASIWEZE MFIKILIA,
BALALA MWANA MVITA ASILIA,

MVITA LEO TWASHANGILIA,
ELIMU BORA IMETUFIKILIA,
SASA TUMETOKA UJAHILIA,
KABISA NYUMA HATUTOANGALIA,

VITIMBI VENU HAVITOMZUILIA,
WALA UONGO WENU MNAOMZULIA,
BALALA MWANZO HUANGALIA,
SIO OVYO KAMA NYIE KUJIKIMBILIA,

ELIMU KWAKE NI KIOO CHA KUJIANGALIA,
YASO MUHIMU MBALI AMEYATUPILIA,
MDA WAKE WOTE KWETU AMEUMALIZIA,
MVITA HAACHI KUTUJULIA,

BALALA KUHUSU ELIMU ATULILIA,
KAMWE MKAZO HAACHI KUTUTILIA,
SASA BUS AMETUNUNULIA,
BASI DUA TWASHINDWA KUMTILIA?

YA ALLAH NAKUOMBA NAKULILIA,
NAJIBU HUSDA ZISIWEZE KUMFIKILIA,
NAO MAHASIDI SHIMO WANALOMTIMBULIA,
WAINGIE WAO NASI TUTAWAFUKILIA,

MAHASIDI WAPI MWAKIMBILIA,
HAMUNA CHOCHOTE CHA KUSHANGILIA,
MVITA BALALA AMEFAGILIA,
NYIE MMEBAKI MWAJILILIA.

Shairi Nime rudi - Posted By Viewer

Leo uwanjani narudi,
jameni sitaki kuwaudhi,
lakini natoa ushahidi,
Balala mejenga yetu biladi,

nyingi siku nimenyamaa,
jameni musikate tamaa,
natafuta wa kumpa mshumaa,
Mombasa izidi kung'aa,

Balala ni Seneta,
Babangida Gavana,
Mahasidi la kunena hawana,
ila kwingi kusonona,

Balala kiongozi shupavu,
enyi musiwe na wivu,
kwani walo wapumbavu,
wataka uongozi kimabavu,

Balala metupa zake sera,
Babangida meshikilia bendera,
nyie mtabaki kujera,
hadi siku ya akhera,

Mwafanya masikhara,
uongozi si mpira,
uongoza ni fikira,
ukicheza utapata izara,

Mimi Ninajbu
nasema Babangida karibu,
Njo uwatie adabu,
hawa waso aibu,

Babangida nakujua
Uongozi wako nautambua,
sera zako si za kubagua,
achana na hawa kichaa wanaugua,

Balala wakawaka,
Babangida wikawika,
Saad shikashika,
Nyinyi ni watu kihakika,

Tamati nimefika,
Balala, Babangida mikono tumewashika,
Saad nae asifika,
Muungwana kihakika,

Mola awatilie baraka,
safari iwe na mwafaka,
Mombasa na yake mipaka,
Muijenge tunavyoitaka,

Balala hoyeee,
Babangida hoyee,
Saad hoyee,
Mombasa hoyee.

Shairi Mvita - Posted By Viewer

SHAIRI LEO NAANDIKA,
JAMENI MUNIPE UHAKIKA,
MAFUTA MUACHE KUNIPAKA,
JE MVITA LEO HAIKUNAWIRIKA?

MVITA ILIKUWA KAMA KICHAKA,
MVITA ILIKUWA KAMA TAKA,
LEO MVITA INASIFIKA,
PWANI NA YAKE MIPAKA,

SERIKALI IKITUMA MAHASIBU,
WAKAGUE MIRADI YA NAJIBU,
HUBAKI HAWANA LA KUJIBU,
WAKIONA MAENDELEO YA TUNAJIBU,

MIRADI MVITA NI NYINGI,
HAO MAHASIBU WAJIONEA MENGI,
WAULIZA LAO GENGI,
MBONA KWETU WABUNGE HAWAJENGI,

WANAFIKI HAWAKOSI LA KUSEMA,
YA NINI JAMENI UHASAMA,
KUMTILIA MJA MWEMA,
HAKUJA ILA KWA WEMA,

BALALA MAENDELEO AMEFANYA,
MIRADI ZAKE ZOTE ZIMEFANA,
WACHA UONGO WEE BWANA,
BALALA AMETUSAIDI KWA MAPANA,

MIAKA ZAIDI YA ARUBAINI,
MVITA IKO HALI DUNI,
WABUNGE MAENDELEO TUMBONI,
WA MVITA WAMEBAKI TAABANI,

LEO BALALA AMEINGIA,
MVITA AKAIANGALIA,
KAAMUA HAWEZI KUVUMILIA,
MPAKA AONE MVITA IMEENDELEA,

SASA TENA BABANGIDA YUWAINGIA,
JAMENI NAWAHAKIKISHIA,
MVITA NA MOMBASA ZITAJIVUNIA,
KUWA NI MIJI BORA KATIKA DUNIA,

TAMATI NIMEFIKA,
NAEEM POKEA SHAIRI ULOITAKA,
MIMI HAPA NINA HAKIKA,
BABANGIDA BALALA WATAVUKA.

Shairi BISMILLAHI NASEMA - Posted By Viewer

BISMILLAHI NASEMA
YA ILAHI MWINGI WA REHMA,
WAJALIE WAJA WAKO WEMA,
MBELE YA WAPENZI KUSIMAMA,

IJUMAA TWAALIKA,
WAPWANI TUTAJUMUIKA,
MOONS UWANJANI TUTAFIKA,
KWA KUDRA ZAKE KARIMA,

BALALA HAJALALA,
WALA HANA MBADALA,
KWA HAKIKA TWAJIVUNIA
BABANGIDA UANJA MEINGIA,

SHEIKH DOR YUKO IMARA,
TUDOR HADI MAKADARA,
WEWE BOSSI TAPATA IZARA,
MWISHOWE UTAPARARA,

ODM KIDETE TULIKITETEA,
KUMBE SHIDA TULIJILETEA,
LAKINI HAKI YETU HAIKUPOTEA,
ODM IMETEKETEA,

BALALA WA MAENDELEO,
TOKA JADI HADI LEO,
TWAMUENZI KILA LEO,
YUKO MBELE KWA KILA TOLEO,

BOSSI JOKA LA MDIMU,
ATEMBEA KAMA WAZIMU,
ENDA AKIHUJUMU,
HAJUI WA KUMLAUMU,

SHEIKH DOR AMEJIPANGA,
UKWELI KWA UWONGO USHAJITENGA,
YU TAYARI AMEJIJENGA,
WEWE UTABAKI KUJINYONGA,

WEWE WAMWITA BALALA FIDHULI,
HUJIONI WEWE MBARADHULI,
UMEKAA KWENYE DHILI,
UNBAKI WAFANYA UDALALI,

MVITA INA WENYEWE,
SISEME YAKO WEWE,
TARATIBU USIRENGEWE,
KAMA KUKU KUMTOROKA MWEWE,

MVITA TWAJIVUNIA,
CABRO ZINAVUTIA
MASHULE ZAJISEMEA,
KLINIKI YAENDELEA,

BALALA NI RAFIKI,
BABANGIDA NI SADIKI,
WEWE NYUMA UTABAKI,
SIPOWACHA UZANDIKI,

BOSSI WAMEKUMILIKI,
HAO WANAFIKI,
USIPOJITENGA NISADIKI,
HAKIKA UTAGHIRIKI,

BABANGIDA KAZI KWAKE,
SHAHBAL HANA CHAKE,
JOHO YUWENDA ZAKE,
UGAVANA SI KITI CHAKE,

BALALA NDIYE SENETA,
KAJEMBE ATAJITAFUTA,
HAONI PA KUPITA,
MWISHOWE TAGONGA UKUTA,

TAMATI NIMEFIKA,
JAPO SIJACHOKA,
NINA MENGI KWA HAKIKA,
SIACHI KUANDIKA,

Shairi - LETU DAIMA MUHIMU.

LETU DAIMA MUHIMU.
..................................

NDUZANGU NAWAAMKIA KWA SALAMU,
KISHA NAWAPA MANENO YALO MUHIMU,
LEO IMEFIKA YETU ZAMU,
KUKIHAMA CHAMA CHA ODMU,

ELFU MBILI WA SABA TULIHUDUMU,
TUMBIONI KAMA WENDAWAZIMU,
NAFSI ZETU TULIZIDHULUMU,
TULIKIONA CHAMA MUHIMU,

KILIKUWA NI KITAMU,
SOTE TULIKOSA FAHAMU,
LEO KICHACHU KAMA NDIMU,
TUMEKUWA NACHO HATUNA HAMU,

TULIKIPENDA MNO WAISILAMU,
WADOGO HATA MAKAMU,
TULIMWAGA ZETU DAMU,
TOKA MOMBASA HADI LAMU,

RAILA ALIKUWA MWALIMU,
NASI TUKAWA WANA WA MWALIMU,
HATUKUJUA KUMBE DHALIMU,
AMEPANGA KUTUDHULUMU,

TULIKIENZI TUKAKIHESHIMU,
TUKAKIONA CHAMA ADHIMU,
KUMBE NI CHAMA HARAMU,
HAKIKA HATUKUKIFAHAMU,

LEO HII YUWAJA HUMU,
NDUGU KUTUTIA SUMU,
TUMEKUWA MAHASIMU,
HATUNA UANADAMU,

KILIPOUNDWA WA KWANZA TULIKIKIRIMU,
TUKAPIGA BARAGUMU,
KUHAKIKISHA KITADUMU,
DAIMA MPAKA DAWAMU,

CHAMA KIMEKUWA CHA KISUMU,
SISI TUKAWA SI MUHIMU,
HATUJUTI HATULAUMU,
TWAJUA ZETU TAIMU,

RAILA POKEA SALAMU,
HII NI TELA SI FILAMU,
MWAKANI MAMBO MAGUMU,
TUTAKUPELEKA KAMA GURUDUMU,

LEO UMEKUWA HASIMU,
BALALA HUMUHESHIMU,
ASAHAUYE UKARIMU,
HAKIKA SI MWANADAMU,

TUNAJIBU SAAD NA IBRAHIMU,
HIYO NDO YETU TIMU,
CHAMA SASA KIMETIMU,
SHEIKH DOR WETU MWALIMU,

JAMENI TUTABASAMU,
MOYO TUSITIE HAMU,
Letu Daima Muhimu,
TUTAKIKOMESHA ODMU.